Daru Makhtutwaat ya Iraq: Atabatu Abbasiyya inamchango mkubwa katika maonyesho ya siku ya nakala-kale za kiarabu

Maoni katika picha
Makamo kiongozi wa Daru Makhtutwaat ya Iraq Dokta Karim Naswifu Jamili amesema kuwa: “Maktaba na Daru Mkhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni, inamchango mkubwa katika maonyesho ya siku ya nakala-kale za kiarabu, imeonyesha malikale za dhamani”.

Akaongeza kuwa: “Jambo la pekee katika tawi lao, vitu vyote walivyo onyesha vipo katika hazina ya Atabatu Abbasiyya, jambo ambalo limethibitisha ukubwa wa hazina yake”.

Kumbuka kuwa maonyesho hayo yalifunguliwa siku ya Jumapili (21 Shabani 1442h) sawa na tarehe (4 Aprili 2021m) kwa lengo la kuangazia utunzaji wa nakala-kale na kuhakikisha haziharibiki.

Atabatu Abbasiyya imewakilishwa na: kituo cha upigaji picha wa nakala-kale na faharasi na kituo cha ukarabati wa nakala-kale na utunzaji wake na kituo cha uhuishaji wa turathi katika Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha habari na utamaduni, wameonyesha malikale na vitu vya kihistoria
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: