Maahadi ya Quráni tukufu inajiandaa kufanya semina za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa wanafunzi wa hauza

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu imetangaza kufanya semina za mwezi wa Ramadhani kuhusu maarifa ya Quráni na kanuni za tajwidi maalum kwa ajili ya wanafunzi wa hauza.

Semina hizo ni sehemu ya mradi wa Quráni kwa wanafunzi wa Dini unaofanywa na tawi la Maahadi katika mji wa Najafu.

Semina inamasharti yafuatayo:

  • 1- Mradi unahusu wanafunzi wa hauza wa ngazi zote waliopo katika mji wa Najafu.
  • 2- Wanafunzi wote wa Dini watakao omba kushiriki, wanatakiwa kutimiza masharti ya kukubaliwa kwenye mradi wa Quráni.
  • 3- Mwanafunzi atakaeomba kushiriki hatakiwi kuwa ameshawahi kushiriki kwenye program hii miaka ya nyuma.
  • 4- Semina zitaanza siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, na itahitimishwa mwezi ishirini na tano, na watafundishwa masomo ishirini.
  • 5- Wanafunzi watakao pata nafasi za kwanza watapewa zawadi ya hela: mshindi wa kwanza atapewa dinari (150,000), na mshindi wa pili dinari (125,000), na mshindi wa tatu dinari (100,000), wanafunzi wote watapewa vyeti vya ushiriki.

Usajili unaendelea hadi tarehe (14 Aprili 2021m).

Kwa maelezo zaidi piga simu namba: 07601683640
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: