Kamati ya majaji wa shindano la kisa kifupi wameanza kuchambua visa vilivyo wasilishwa kwao

Maoni katika picha
Kamati ya majaji wa shindano la kitaifa linalo fanywa kwa njia ya mtandao la kisa kifupi kwa wanafunzi wa sekondari (upili), lililo andaliwa na idara ya uhusiano wa vyuo na shule katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kuchambua visa vilivyo wasilishwa kwao siku ya Ijumaa asubuhi mwezi (26 Shabani 1442h) sawa na tarehe (9 Aprili 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) katika Ataba tukufu.

Kiongozi wa idara ya harakati za shule amesema kuwa: “Baada ya kumaliza kupokea visa zaidi ya (40) kutoka kwa wanafunzi wa shule tofauti hapa Iraq, kamati ya majaji imeanza kuzichambua kwa kuzingatia kanuni na masharti ya shindano, hadi vibaki visa bora kumi, miongoni mwa majaji wanaoshiriki katika kuchambua visa hivyo ni Ustadh Hassan Shawili mkuu wa idara ya michezo na mkufunzi katika wizara ya malezi, chini ya usimamizi wa Ustadh Hussein Khabbaaz na Ustadh Hashim Swafaar kutoka kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Kamati itamaliza kazi yake asubuhi ya Jumamosi na matokeo yatatangazwa mubashara kupitia ukurasa wa mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel na kwenye mtandao wa kimataifa wa Alkafeel baada ya saa nane siku hiyo”.

Kumbuka kuwa shindano hili ni sehemu ya harakati za mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, aidha ni sehemu ya harakati za Ataba katika mazingira haya magumu, inatumia njia mbadala kuendeleza shughuli za kitamaduni kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii, kwa namna ambayo inaongeza kiwango cha ubunifu kwa wanafunzi, na kuwajengea moyo wa kushindana katika kuibua vipaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: