Mkuu wa mkoa wa Karbala: Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesaidia kuboresha sekta ya kilimo

Maoni katika picha
Mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Khatwabi, amesema kuwa miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha sekta ya kilimo.

Katika ziara aliyofanya siku ya Jumamosi kwenye baadhi ya mashamba ya Atabatu Abbasiyya tukufu akasema: “Mashamba ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni miradi yenye mafanikio makubwa katika mkoa wa Karbala, miradi hiyo inasaidia kujitegemea wenyewe katika soko”.

Akasema: “Tunaunga mkono juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye miradi hii, pongezi za pekee ziwafikie watendaji wa mashamba haya, kwani mafanikio yao yanaleta mabadiliko katika sekta ya kilimo, kwenye mazao ya kimkakati na mengineyo”.

Bwana shamba wa Karbala tukufu Mhandisi Razaaq Twaaiy akasema: “Katika ziara yetu ya leo pamoja na mkuu wa mkoa, tumeona maendeleo makubwa katika mashamba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeona mafanikio mazuri yanayo letwa na watumishi wa mashamba hayo”.

Akasema: “Katika kuonyesha uungaji mkono wetu kwenye miradi hii, tutatuma jopo la wataalamu wetu watakao kuja kutoa ushauri wa kitaalam pamoja na kuwaunganisha na wizara ya kilimo ili kutafuta soko la mazao haya na kuhakikisha wanakua wazalishaji wakubwa hapa nchini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: