Juhudi kubwa ya kuhifadhisha kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
Idara ya tahfidhi katika Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad, inafanya juhudi kubwa ya kuhifadhisha kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, kupitia semina mbalimbali zinazo fanywa chini ya walimu wa tahfidhi.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Ali Khalidi ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu juhudi zinazo fanywa na idara hiyo, amesema kuwa: “Tangu kufunguliwa kwa idara ya tahfidhi katika tawi la Maahadi ya Bagdad mwaka (2014) imekua ikifanya semina za kuhifadhisha Quráni katika maeneo tofauti ya Bagdad, hasa katika eneo la Karkha na Raswaafah”.

Akaongeza kuwa: “Tuna walimu wengi walio bobea katika masomo ya tahfidhi, walio hitimu tahfidhi kwao watu wengi wa Bagdad”.

Akasema: “Idara hufanya semina zake kwa kufuata ratiba ya Maahadi ya Quráni tukufu ya Atabatu Abbasiyya”.

Akaendelea kusema: “Pembezoni mwa semina za tahfidhi huwa tunafanya vikao vya usomaji wa Quráni kwa wanafunzi wa tahfidhi, asilimia kubwa ya wanafunzi wetu hupata ushindi katika mashindano ya Quráni ya kitaifa na kimataifa”.

Akasema: “Wakati wa kipindi cha janga la Korona idara imekua ikifanya semina kwa njia ya mitandao mbalimbali ya mawasiliano”.

Tambua kuwa Maahadi ya Quráni tukufu ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na inalenga kueneza elimu ya Quráni na kuandaa jamii inayo fanyia kazi mafundisho ya Quráni na yenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta tofauti za Quráni takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: