Kituo cha utamaduni wa familia kinajiweka wazi katika uwanja wa sekula

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na kitengo cha uelekezaji wa nafsi na muongozo wa malezi katika chuo kikuu cha Al-Ameed, wameandaa nadwa waliyo ipa jina la: (changamoto za kinafsi katika zama za janga la Korona), ambayo imelenga watumishi wa chuo, nadwa hii inafanywa kwa ushirikiano wa taasisi za Atabatu Abbasiyya tukufu.

Bibi Asmahani Ibrahim mkuu wa kituo cha utamaduni wa familia ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Nadwa hii ni sehemu ya harakati za kituo, tunashirikiana na vyuo vikuu vingi, kikiwemo chuo kikuu cha Al-Ameed, kwa ajili ya kunufaika na uzowefu walio nao watumishi wa kituo, na kufungua milango ya ushirikiano, nadwa hii itaimarisha ushirikiano wa kuendelea kufanya nadwa za kitamaduni kwa faida ya mwanamke na taasisi za kimalezi na kielimu”.

Akaongeza kuwa: “Mtoa mada wa nadwa hii alikua ni mtaalamu wa tiba ya nafsi Ustadhat Adhraau Abbasi Shami, ameeleza mambo mengi kuhusu changamoto za familia na namna ya kuzitatua katika mazingira ya janga hili la Korona bila kupata madhara”.

Kumbuka kuwa kituo cha utamaduni wa familia kinalenga kutatua changamoto za familia na kuleta utulivu wa nafsi ndani ya familia, kilianzishwa kutokana na wingi wa changamoto zilizopo katika familia za wananchi wa Iraq, zinazo athiri utulivu wa nafsi kwa mtu na jamii, kimefanya kazi kubwa katika kutekeleza malengo yake kupitia nadwa na warsha mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: