Maqaamu ya Imamu Mahadi (a.f) imekuwa mwenyeji wa kisomo cha Quráni mwezi mzima wa Ramadhani

Maoni katika picha
Quráni tukufu inasomwa kila siku katika mwezi huu mtukufu ndani ya moja ya kumbi za Maqaamu ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na Daarul-Quráni tukufu, kisomo hicho kimeanza tangu siku ya kwanza ya mwezi huu mtukufu na kitaendelea hadi mwisho wa mwezi.

Kiongozi wa Maqamu hiyo bwana Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kisomo cha Quráni kinacho fanywa katika Maqaamu tukufu, ni moja ya visomo vingi vya Quráni vinavyo fanywa na Maahadi ya Quráni chini ya Atabatu Abbasiyya, imeandaliwa sehemu maalum ya kusomea Quráni ambapo ukaaji wa umbali kati ya mtu na mtu umezingatiwa pamoja na tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ikiwa ni pamoja na kuweka idadi maalum ya washiriki”.

Akaongeza kuwa: “Quráni inasomwa kila siku baada ya swala ya Adhuhuri, na itaendelea hivyo hadi mwisho wa mwezi huu mtukufu, kila siku linasomwa juzuu moja, husoma mtu mmoja mmoja kwa kupokezana, upanuzi mpwa wa Maqaam umesaidia usomaji huu, kwa kupatikana sehemu kubwa iliyo kando ya kumbi zingine, pamoja na uwezekano wa kutekeleza masharti ya kujikinga na maambukizi”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu imeandaa ratiba maalum ya usomaji wa Quráni katika mwezi huu wa Ramadhani, yenye vipengele vingi, chini ya utekelezaji wa kanuni za kujikinga na maambukizi, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni usomaji wa Quráni tukufu, na kuibua vipaji vya usomaji wa Quráni pamoja na kuviendeleza, na kunufaika na mazingira mazuri ya kiroho yanayo patikana katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: