Chuo kikuu cha Al-Ameed kimevishinda vyuo binafsi vya Karbala na vyuo vya serikali katika ufundishaji wa kielektronik (masafa)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa, kimepata nafasi ya kwanza katika ufundishaji bora kwa njia ya mtandao miongoni mwa vyuo vya serikali na binafsi mkoani Karbala, kwa mujibu wa ripoti iliyo tolewa na kituo cha kitaifa cha taaluma bora chini ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, pamoja na kituo cha chuo cha teknolojia taaluma na mawasiliano.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo chuo kikuu cha Al-Ameed kimepata nafasi ya kwanza kwenye sekta ya ufundishaji kwa njia za mitandao miongoni mwa vyuo za serikali na binafsi katika mkoa wa Karbala, ripoti imeonyesha mafanikio ya vituo nane katika vyuo vikuu nane, huku vituo viwili vikiwa vinaelekea kufanikiwa kutoka katika vyuo binafsi vya Iraq.

Rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali ameshukuru na kupongeza ripoti hiyo, aidha amewashukuru watu wote walio changia mafanikio hayo kwenye kituo cha ufundishaji kwa njia ya mtandao katika chuo kikuu cha Al-Ameed, na kukifanya kupata nafasi ya kwanza katika mkoa mtukufu wa Karbala, mafanikio haya yamesababishwa na kazi kubwa pamoja na juhudi ya hali ya juu iliyofanywa na wakufunzi wetu, walio jitolea kufundisha kwa bidii katika kipindi hiki cha janga la virusi vya Korona, lililo athiri sekta ya elimu kwa kiwango kikubwa.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kimejiwekea mikakati ya kwenda sambamba na maendeleo ya kielimu, na kutumia njia za kisasa zaidi katika ufundishaji, na kuhakikisha matokeo yake yanaonekana bayana kwa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: