Zawadi na nadhiri.. hupokelewa vipi? Aaina gani? Hupelekwa wapi?

Maoni katika picha
Kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefafanua utaratibu unaotumika kupokea zawadi na nadhiri zinazo kabidhiwa katika Ataba tukufu, sawa ziwe mali au thamani pamoja na kueleza namna zinavyo tumika.

Rais wa kitengo Sayyid Muiin Husseini amesema: “Baadhi ya waumini wanaweza kujiuliza kuhusu utaratibu unaotumika kukusanya zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na aina za matumizi yake, wakati mwingine huwa tunaulizwa maswali hayo moja kwa moja na mazuwaru wa Atabatu Abbasiyya tukufu au kwa njia ya barua, pamoja na njia za mitandao ya kijamii, tunapenda kubainisha kuwa zawadi na nadhiri hupokelewa na idara maalum iitwayo (idara ya upokeaji), hupokea zawadi na kutumiwa kama anavyo taka mtoaji, baada ya kupokea kitu chochote huandikwa kwenye daftari maalum na mtoaji hupewa risiti, kisha mali hiyo huwasilishwa kwa mhazini mwenye mafungamano na kitengo cha mali, inapokuwa iliyo kabidhiwa ni pesa au mali ya kuhamishika”.

Akafafanua kuwa: “Zawadi zimegawanyika sehemu tatu, ambazo ni: pesa, vitu vya thamani, kama dhahabu na madini mengine, miswala na vinginevyo, aina ya tatu ni wanyama wa kuchinja, kanuni zaote za afya huzingatiwa pamoja na kanuni za kisheria, wanyama hao hukabidhiwa rasmi kwenye mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kuwa kitengo cha kupokea zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo muhimu sana, kutokana na uhusiano wake wa moja kwa moja na mazuwaru, kwani hupokea zawadi na nadhiri kutoka kwa mazuwaru watukufu chini ya kanuni zilizo wekwa, sambamba na kuwapa baadhi ya zawadi za kutabaruku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: