Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa futari kwa wahudumu wa mawakibu Husseiniyya katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili Tukufu, kinatoa futari kwa wahudumu wa mawakibu Husseiniyya za Karbala ndani ya mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Riyadh Niímah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Miongoni mwa ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kukaribisha wageni tofauti katika mwezi huu mtukufu, miongoni mwa wageni hao ni watoa huduma wa mawakibu Husseiniyya, pamoja na kuendelea kuwasiliana nao na kujadili mambo yanayo wahusu, na kufanya kazi kwa ushirikiano baina yao hususan wakati wa ziara na matukio ya kidini, pamoja na kujadili mambo yatakayo saidia kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo kinafanya kazi mwaka mzima pamoja na watoa huduma wa mawakibu Husseiniyya, aidha hufanya vikao maalum, kikiwemo hiki ambacho hufanywa kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani, tunaweza kusema ni utamaduni wa kitengo hiki pamoja na watumishi wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho kinawajibika kuratibu kazi za vikundi na mawakibu Husseiniyya, na kutoa vitambulisho kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ndani na nje ya Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: