Kuendelea kwa vikao vya usomaji wa Quráni vya wanawake

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kufanya vikao vya usomaji wa Quráni vya wanawake ndani ya mwezi wa Ramadhani, ambavyo vilianza tangu siku ya kwanza ya mwezi huu mtukufu na vitaendelea hadi mwisho wa mwezi, ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) chini ya utekelezaji wa masharti ya kujikinga na maambukizi.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi, akaongeza kuwa: “Hakika usomaji huu wa Quráni hufanywa kila mwaka ndani ya mwezi huu mtukufu wa Quráni, ni utamaduni ulio zoweleka, lakini mwaka huu kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, tumetosheka na vikao viwili tu, kimoja tunasoma asubuhi na kingine jioni, wanashiriki watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kundi la mazuwaru”.

Akaendelea kusema: “Tunakikoa kingine cha usomaji wa Quráni katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) asubuhi na jioni, kuna mazingira mazuri ya kiroho yanayo endana na utukufu wa mwezi huu, kuna usomaji kwa njia ya mtangao pia sambamba na maswali ya Quráni na Aqida, ili kufanya mazingatio na tafakuri”.

Kumbuka kuwa idara ya Quráni inaharakati zinano hudhuriwa na washiriki moja kwa moja na zinazo fanywa kwa njia ya mtandao, kama usomaji wa Quráni na maadhimisho mbalimbali ndani ya mwaka mzima, chini ya misingi ya mwanamke wa kiislamu na misingi ya Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: