Wito wa kuhudhuria nadwa ya pili kwa viongozi wa Dini na athari zao katika kutatua changamoto za kibinaadamu

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa wito kwa watafiti na wasomi wa kuhudhuria nadwa ya pili miongoni mwa nadwa za (viongozi wa Dini na athari zao katika kutatua changamoto za kibinaadamu), inayo simamiwa na kituo cha tafiti za kiislamu kwa kushirikiana na jumuiya ya kielimu Al-Ameed. Nadwa ya pili itakua na anuani isemayo: (Misingi ya mafundisho ya Ahlulbait –a.s- na uhusiano na wengine), watoa mada ni Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Ashkuri na Mheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum, walimu wa hauza, nadwa itafanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Imamu Murtadha (r.a) katika mji wa Najafu, siku ya Jumapili mwezi kumi na mbili Ramadhani tukufu (1442h) sawa na tarehe (25 Aprili 2021m), saa tatu jioni kupitia jukwaa la (zoom) kwa link ifuatayo: https://us02web.zoom.us/j/3740873005
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: