Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu unatembelea familia za waathirika wa tukio la hospitali ya ibun Khatwibu

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, asubuhi ya leo mwezi kumi na tatu Ramadhani (1442h) sawa na (26 Aprili 2021m), umetembelea waathirika wa tukio la moto uliotokea katika hospitali ya ibun Khatwibu mkoani Bagdad, na kutoa pole kwa janga hilo.

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Jawaad Hasanawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ujumbe kutoka Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya umetembelea waathirika wa tukio la moto wa jana katika hospitali ya ibun Khatwibu Bagdad na kutoa pole kwa wahanga hao”.

Akaongeza kuwa: “Hospitali ya rufaa Alkafeel katika mji wa Karbala inapokea majeruhi wa tukio la moto wa jana, watatibiwa na kupewa huduma zingine bure, kwa ruhusa ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: