Furaha imetanda katika kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Almujtaba

Maoni katika picha
Furaha imetanda katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yamewekwa mapambo ndani ya nje ya korido zake, katika kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), ambaye alizaliwa siku kama ya kesho mwezi kumi na tano Ramadhani.

Mauwa ya rangi na aina tofauti yamewekwa ndani na nje ya haram takatifu, pamoja na mabango yanayo onyesha baadhi ya utukufu na sifa za Imamu Hassan Almujtaba (a.s), sambamba na kupamba kuta za haram kwa taa za rangi kama ishara ya kuadhimisha siku ya mwezi kumi na tano Ramadhani.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu huandaa ratiba maalum ya kuadhimisha tukio hili kila mwaka, huwa na vipengele tofauti baadhi yake huendelea kwa muda wa siku tatu, kama vile kongamano la kuadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ambalo hufanywa katika mji wa Hillah, na lingine hufanywa ndani ya haram tukufu, lakini kutokana na mazingira ya mwaka huu na kuheshimu maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo himiza kujiepusha na mikusanyiko ya watu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, tumelazimika kutosheka na baadhi ya program zinazo endeshwa kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: