Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu unatembelea watu walio jeruhiwa katika tukio la moto uliozuka kwenye hospitali ya ibun Khatwibu na umeahidi kuwasaidia

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya umetembelea majeruhi wa tukio la moto uliozuka katika hospitali ya ibun Khatwibu, walio lazwa kwenye hospitali tofauti za mji mkuu wa Bagdadi, asubuhi ya Jumanne mwezi (14 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (27 Aprili 2021m), baada ya kumaliza kutembelea na kuwapa pole ndugu wa marehemu waliofariki kutokana na tukio hilo hapo jana.

Kwa mujibu wa maelezo ya muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya na makamo rais wa kitengo cha Dini Shekh Aadil Wakili amesema: “Ziara hii ya kutembelea majeruhi wa tukio hilo la kuhuzunisha, lililo athiri asilimia kubwa wa wagonjwa waliokua wamelazwa katika hospitali ya ibun Khatwibu, tumeifanya chini ya maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, tumeanza kuwatembelea wafiwa na kuwapa pole kisha tunatembelea wagonjwa waliolazwa hospitalini na wanaotibiwa majumbani kwao, kwa ajili ya kuwajulia hali na kuwasaidia”.

Akaongeza kuwa: “Aidha tumewasomea dua na kuwafikishia salamu kutoka kwa watumishi wa malalo mbili takatifu chini ya viongozi wakuu wa kisheria, pamoja na kuwaambia utayali wetu wa kusaidia matibabu kwa majeruhi na kuwahamishia kwenye hospitali zilizo chini ya Ataba mbili katika mkoa wa Karbala, tumewapa zawadi za kutabaruku kutoka kwenye malalo mbili tukufu, ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Majeruhi na familia zao wameshukuru sana kuja kuwajulia hali, wakauambia ugeni ulio watembelea hali yao na shukrani zao kwa viongozi wa Ataba mbili tukufu kwa namna unavyo wajali na kuwasaidia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: