Wito wa kushiriki katika shindano la Baraaimu za mwezi wa kheri

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza kwa shindano maalum la mwezi wa Ramadhani la watoto wa (kiume na wa kike) ambao bado hawajafikia umri wa kuwajibikiwa na sheria na shindano hilo limepewa jina la (Baraaimu za mwezi wa kheri).

Kwa lengo la kushajihisha kufunga katika siku za mbele kwa kundi hilo la watoto na kuwajulisha utukufu wa funga kwa njia rahisi kwao, na kuwafanya kuwa tayali kutekeleza ibada hiyo watakapo fika umri wa kuwajibikiwa na sheria.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kituo bibi Asmahani Ibrahim, akasema: “Shindano hili ni moja ya harakati zinazo fanywa na kituo chetu tangu mwezi wa Ramadhani ulipoingia, kwa ajili ya kunufaika na mazingira mazuri ya kiroho yaliyopo katika mwezi huu, harakati zenu zinalenga watu wa rika zote, tunaharakati za uelekezaji, utamaduni, malezi, elimu na Dini”.

Akaendelea kusema: “Katika shindano hili tumelenga kundi la watoto, ambalo tunaamini kuwa ni kundi muhimu linalo takiwa kupewa kipaombele na kuwaandaa kwa ajili ya hatua muhimu katika maisha yao, ambayo ni hatua ya kwajibikiwa na sharia, na kuwajengea mazingira ya kufanya ibada ikiwemo funga, shindano hili litasimamiwa na kamati ya wataalamu”.

Kwa yeyote anayetaka kushiriki ajiunge kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/rjLNdzHYKxcnPWJh6
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: