Mahafali za vikao vya usomaji wa Quráni katika kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha Maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa hafla ya usomaji wa Quráni katika wilaya ya Hindiyya kama sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume Imamu Hassan Almujtaba (a.s), hafla hiyo imefanywa ndani ya Maqaam ya Sayyid Ahmadi bun Imamu Mussa Alkaadim (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la waumini sambamba na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi.

Kiongozi wa tawi la Maahadi Sayyid Haamid Marábi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Hafla hii ni sehemu ya ratiba ya kuadhimisha siku hizi tukufu, ambapo kuna kipengele cha kuadhimisha mambo yaliyo tokea katika mwezi huu, likiwemo swala la kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait (a.s) Imamu Hassan Almujtaba (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu kisha yakafuata mawaidha, mzungumzaji ameongea kuhusu mafundisho yanayo patikana katika maisha ya Imamu Hassan (a.s) kijamii na kisiasa, baada ya mawaidha zikafuata kaswida na mashairi kuhusu kuwapenda Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, linafanya harakati mbalimbali zinazo husu Quráni katika wilaya ya Hindiyya mashariki ya mkoa wa Karbala, pamoja na miradi tofauti inayo lenga kufundisha ujumbe wa vizito viwili vitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: