Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imewekwa mapambo meusi

Maoni katika picha
Kuta za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimewekwa mapambo meusi pamoja na mabango yanayo ashiria huzuni, kwa ajili ya kukumbuka msiba mkubwa zaidi uliotokea katika familia ya Mtume Muhammad (a.s) baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), hizi ni siku za huzuni iliyo anza kwa tukio la kujeruhiwa kiongozi wa waumini (a.s) tarehe kumi na tisa Ramadhani hadi kufariki kwake tarehe ishirini na moja mwezi huu.

Makamo rais wa kitengo cha uangalizi wa haram tukufu Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wetu wameweka mapambo meusi na mabango yanayo onyesha huzuni na maombolezo ya kifo cha pambo la Dini na kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s)”.

Akasema: “Tumeweka mabango matatu makubwa katika sega la dhahabu tukufu, pamoja na kuweka mabango mengine ndani ya haram na kwenye milango yanayo ashiria huzuni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: