Wito wa kushiriki katika shindano maalum la (Hadi kuchomoza Alfajiri) kwa watoto

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa wito wa kushiriki kwenye shindano la (hadi kuchomoza Alfajiri) kwa watoto wenye umri chini ya miaka nane, linalo husu kuhifadhi surat Fajri na kuisoma kwa usahihi.

Kiongozi wa kituo bibi Asmahani Ibrahimu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hili ni moja ya mashindano mengi yaliyo fanywa na kituo ndani ya mwezi huu mtukufu, kwa kutumia majukwaa ya mitandao, tumekuwa na mashindano ya aina tofauli yaliyo husisha watu wa makundi mbalimbali katika jamii, miongoni mwa makundi hayo ni kundi la watoto, na hili ni moja kati ya mashindano hayo”.

Akaongeza kuwa: “Namna ya kushiriki kwenye shindano hili ni kutuma picha ya video, pamoja na kutaja jina la mshiriki kwenye link ya shindano. Tarehe ya mwisho ya kupokea video za washiriki ni mwezi thelethini Ramadhani, washindi watatangazwa baada ya majaji kumaliza kazi ya kusahihisha na kupangilia matokeo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: