Katika malalo za watoto wake: Mawakibu za waombolezaji zinaomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s)

Maoni katika picha
Mawakibu za watu wa Karbala zimeomboleza msiba mkubwa uliotokea katika nyumba ya Mtume katika siku kama hizi, kifo cha kiongozi wa waumini na kipenzi wa wachamungu Ali (a.s), mbele ya malalo za watoto wake Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s), zilianza kumiminika tangu siku aliyo jeruhiwa hadi siku aliyo kufa kishahidi.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan kwa mtandao wa Alkafeel, amesema: “Hakika uombolezaji wa msiba huu ambao huzingatiwa kuwa msiba mkubwa zaidi baada ya msiba wa kufiwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w), huchukuliwa kuwa utamaduni wa watu wa Karbala, sawa iwe kwenye msiba huu au misiba mingine ya vifo vya Maimamu watakatifu (a.s), wamerithishana kizazi baada ya kizazi”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo hiki na watumishi wake wameandaa ratiba ya kupokea mawakibu za waombolezaji zinazo kuja baada ya wakati wa futari, zimepangwa njia wanazo pita pamoja na kuainisha sehemu ya kuanzia matembezi na sehemu ya kumalizia, pamoja na kuzingatia masharti yote ya kujikinga na maambukizi, na kuhakikisha hakuna msongamano mkubwa wa watu wala muingiliano wa mawakibu, tumeweka watumishi wanao simamia zowezi hilo sehemu zote zinakopita mawakibu, kuanzia mwanzo hadi mwisho”.

Salmaan akamalizia kwa kusema: “Maukibu zote zitakusanyika katika siku ya kifo chake chini ya jina moja la (maukibu ya watu wa Karbala ya pamoja) na kufanya ziara kwa pamoja katika malalo mbili takatifu, kisha zitaondoka Karbala kuelekea Najafu kumpa pole kiongozi wa waumini (a.s), Ataba mbili zitagharamia kusafirisha waombolezaji na kuwapa mahitaji yote ya lazima”.

Kumbuka kuwa mawakibu hizi huanza matembezi yake katika barabara zinazo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kuzunguka malalo hiyo huku wakiimba kaswida za huzuni na kuomboleza, huelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya malalo mbili takatifu, huku wakiimba na kupiga matam hadi ndani ya haram ya Imamu ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: