Maahadi ya Quráni inafanya nadwa ya tabia njema za mwananchi kwa mujibu wa Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya inafanya nadwa yenye anuani isemayo: (Tabia njema za mwananchi chini ya muongozo wa Quráni), katika wilaya ya Mahawil, na kufuata tahadhari za kujikinga na maambukizi.

Wameangalia aya za Quráni tukufu zinazo zungumzia jamii, mzungumzaji alikua ni Dokta Haidari Shalaah mmoja wa wakufunzi wa chuo kikuu cha Baabil/ kitivo cha elimu za kiislamu.

Hii ni moja ya nadwa zilizofanywa na Maahadi katika mkoa wa Baabil, katika harakati zake za mwezi mtukufu wa Ramadhani, zinazo lenga vijana na makundi ya watu wengine katika jamii.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya harakati nyingi katika mwezi huu wa Ramadhani, kama sehemu ya kuuenzi mwezi huu na kueneza elimu katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: