Maahadi ya Quráni imekamilisha semina maalum katika wilaya ya Hindiyya

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imekamilisha semina maalim ya Quráni iliyo pewa jina la Imamu Hassan (a.s), iliyokuwa na masomo ya Quráni, Aqida na Fiqhi, pamoja na masomo ya awali katika kuhifadhi na kusoma Quráni tukufu.

Masomo yamedumu kwa muda wa miezi mitatu mfululizo, washiriki walikua zaidi ya wanafunzi (20), chini ya ukufunzi wa walimu waliobobea katika masomo ya Quráni, semina hiyo ilikua inalenga kutengeneza jamii yenye uwelewa wa Quráni na kuvitambua vyema vizito viwili.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu ni moja ya sehemu muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na inalenga kufundisha elimu ya Quráni na kusaidia kutengeneza jamii ya watu wenye uwelewa wa Qur,ani na uwezo wa kufanya tafiti mbalimbali za maarifa ya Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: