Kikosi cha Abbasi (a.s) kinaratibu shughuli ya kutoa damu

Maoni katika picha
Wahudumu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mkoa wa Basra, kimeandaa mpango wa kutoa damu katika kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Shughuli hii imeratibiwa kwa kushirikiana na benk ya damu ya mkoa, akaongeza kuwa kikosi kinaendelea kutoa huduma mbalimbali na misaada ya kibinaadamu katika mkoa wa Basra.

Mkuu wa benk ya damu katika mkoa wa Basra amewashukuru viongozi wa kikosi hicho, akasema kuwa hili sio jambo geni kwao, kwani wamekua mstari wa mbele daima katika kuhudumia jamii, kupitia miradi tofauti ya kibinaadamu katika mkoa wa Basra na mikoa mingine ya Iraq.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinafanya miradi mbalimbali ya kibinaadamu tangu lilipo tangazwa janga la virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na shughuli za kupuliza dawa na kujenga kituo cha (Yaasin) katika mkoa wa Karbala kwa ajili ya kufanya shughuli za maziko kwa watu waliokufa na maradhi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: