Rais wa chuo kikuu cha Alkafeel ameonyesha mafanikio ya elimu masafa

Maoni katika picha
Dokta Nuris Dahani Rais wa chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ameeleza hatua iliyopigwa na chuo hicho katika utoaji wa elimu pamoja na changamoto ya uwepo wa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, na njia wanazotumia kuwasilisha mada za masomo kwa wanafunzi kwa urahisi kwa kutumia nyenzo za kisasa, na jinsi walivyo fanikiwa kuweka mazingira bora ya usomaji na usomeshaji.

Ameyasema hayo katika kongamano la kimataifa la awamu ya pili kuhusu usomaji kwa njia ya mtandao (elimu masafa), lililo andaliwa na idara ya utafiti na maendeleo katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu/ kikosi cha wizara kinacho husika na elimu kwa njia ya mtandao (elimu masafa), chini ya kauli mbiu isemayo (Tuondoe umbali) lililofanywa kwa kutumia jukwaa la (ZOOM) jana Ijumaa (24 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (7 Mei 2021m).

Katika kikao cha kwanza Dahani ameeleza hali halisi ya ufundishaji kwa njia ya mtandao katika taifa la Iraq kwa ujumla na katika chuo kikuu cha Alkafeel kwa namna ya pekee, kwa kuwa chuo kikuu Alkafeel kinamaendeleo makubwa ya ufundishaji wa kutumia njia ya mtandao hapa Iraq, kinavifaa vya kisasa na wataalamu wa kutosha, kama mfumo wa sauti, kamera na mitambo mingine ambayo imewasaidia wanafunzi kuvuka salama katika kipindi hiki cha janga la virusi vya Korona mwaka jana na mwaka huu.

Kumbuka kuwa ameshiriki katika kikao cha kwanza cha kongamano hilo na mhadhara wake kufuatiliwa na zaidi ya washiriki elfu moja miatano kutoka ndani na nje ya Iraq, maoni mbalimbali yametolewa na washiriki wakati akiongelea vyuo vikuu vya Iraq na uhusiano wake na vyuo vingine duniani kwa ajili ya kufikia malengo ya kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: