Wanajeshi wanashiriki katika usomaji wa Quráni ndani ya mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Polisi na wanajeshi wa Karbala wanashiriki katika vikao vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi wa Ramadhani vinavyo simamiwa na Maahadi ya Quráni chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkuu wa Maahadi Shekh Jawadu Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Usomaji wa Quráni ni moja ya jambo muhimu ndani ya mwezi huu mtukufu, askari hupewa nafasi ya kushiriki, mwaka huu kutokana na kuwepo kwa janga la Korona, tumetenga sehemu ndani ya moja ya sardabu za Atabatu Abbasiyya tukufu na kutosheka na idadi maalum ya wasomaji, ambapo husomwa juzuu moja kila siku”.

Akaongeza kuwa: “Lengo la ushiriki huu ni kusambaza ujumbe wa amani duniani kote, na kuwajulisha kuwa wanaolinda waislamu ni watu wa Quráni na wanajua mafundisho ya Quráni, vifua vyao vimejaa nuru ya kitabu hicho, pamoja na kutia hofu na uwoga katika nyoyo za maadui”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwaka mzima hufanya semina nyingi za Quráni tukufu, kikiwemo kisomo hiki ambacho hufanywa kila mwaka ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kutokana na uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona tumetosheka na aina hii ya usomaji kama tulivyo fanya mwaka jana, kisomo hicho kinarushwa kila siku saa kumi na moja jioni kwenye luninga tofauti, kupitia masafa ya bure iliyo tengenezwa na kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii, kila siku tunasoma juzuu moja kwa usomaji wa kidogokidogo kila mtu, na hutumia muda wa saa moja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: