Husseiniyya na majengo ya Samawa yamejaa vikao vya usomaji wa Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa tawi lake katika mkoa wa Muthanna na kituo chake cha Samawa wameratibu vikao mbalimbali vya usomaji wa Quráni tukufu vinavyo fanywa ndani ya Husseiniyya na kwenye majengo tofauti chini ya usimamizi wa jopo la wasomi wa Quráni, na kuhudhuriwa na vikundi vya watu wa Samawa wakiwa wamechukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Mkuu wa Maahadi hiyo, Shekh Jawadi Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika vikao vya usomaji wa Quráni ni sehemu ya mkakati tulio weka katika mwezi huu mtukufu, mwezi wa Quráni, vikao hivyo vinafanywa katika kituo cha Maahadi na kwenye matawi yake, miongoni mwa matawi hayo ni hili la mkoani Muthanna”.

Akaongeza kuwa: “Wasimamizi wa tawi la Maahadi walikua wamesha jiandaa kufanya kisomo hiki, waliandaa kundi la wasomaji wa Quráni pamoja na kuainisha majengo na Husseiniyya zitakazo tumika kwa ajili ya usomaji huo, sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, vikao hivyo vya usomaji wa Quráni vimepata muitikio mkubwa, pamoja na kuwepo kwa idadi maalum inayo ruhusiwa kushiriki kutokana na mazingira ya afya kwa sasa”.

Kumbuka kuwa matawi ya Maahadi ya Quráni tukufu katika mkoa wa Karbala, yameanza ratiba ya usomaji wa Quráni ndani ya Husseiniyya na mazaru chini ya tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: