Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati kimehitimisha nadwa zake za mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimekamilisha nadwa zilizo pewa jina la (Viongozi wa Dini na athari yao katika kutatua changamoto za kibinaadamu), kwa kushirikiana na kitivo cha sayansi ya kiislamu katika chuo kikuu cha Waarithul-Ambiyaa (a.s).

Katika nadwa ya tatu na ya mwisho iliyopewa jina la (Mustakbali wa mahusiano ya viongozi wa Dini na jinsi ya kunufaika nayo), mtoa mada alikuwa ni Mheshimiwa Sayyid Rashidi Husseini mwalimu wa Hauza, na Dokta Twalaal Kamali mkuu wa kitivo cha sayansi ya kiislamu katika chuo kikuu cha Waarithul-Ambiyaa (a.s).

Wazungumzaji wameeleza nafasi ya roho, maadili na jamii katika kuondoa utengano wa wanaadamu na kujenga tabia ya kuheshimiana, na msingi ubakie kuwa ni ushirikiano wa kibinaadamu, wakabainisha kuwa miradi yote ya kiaskari, kisiasa na kikoroni; pamoja na kitamaduni na kiuchumi ni tatizo kwa wanaadamu wote.

Ilitolewa nafasi ya kujadili kwa pamoja kati ya wahadhiri na washiriki, ambapo wahadhiri walijibu maswali na kufafanua zaidi palipohitaji ufafanuzi, nadwa hizi ni sehemu ya harakati za idara ya nadwa na masomo katika kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati, wameongea mambo muhimu katika jamii.

Kumbuka kuwa nadwa imefanywa ndani ya jengo la Imamu Murtadha (a.s) katika mji wa Najafu, na kuhudhuriwa na watu wengi wasomi wa hauza na sekula kutoka vyuo tofauti vya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: