Maahadi ya Quráni tukufu katika mkoa wa Baabil imehitimisha mashindano ya (maneno ya nuru) yaliyofanywa kupitia redio

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya, imehitimisha mashindano la (maneno ya nuru) yaliyofanywa kupitia redio katika mwezi wa Ramadhani, kwa kushirikiana na idhaa ya Babeliyuun.

Mashindano yamefanywa ndani ya mwezi mtukufu, yalikuwa yanatangazwa mubashara (moja kwa moja), chini ya Ustadh Luaiy Watwifi kiongozi wa idara ya usomaji katika tawi la Maahadi na jopo makini la majaji, aliye andika alama za hukumu za usomaji ni kiongozi wa tawi Sayyid Muntadhir Mashaikhiy, na hukumu za kusimama na kuanza Ustadh Nabiil Asadiy, na hukumu za tafsiri Shekh Hassan Maámuuri.

Mshindi wa kwanza katika usomaji alikuwa ni Ahmadi Asadiy na mshindi wa pili ni Bahaau Ali Jaabir, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Abbasi Ali Shiyaai.

Tambua kuwa shindano lilikuwa linahusu hukumu za usomaji, kusimama na kuanza, washindi wa usomaji na tafsiri wamepatikana kwa kupiga kura kati ya wenye majibu sahihi.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Quráni katika mkoa wa Baabil linaharakati mbalimbali zinazo husu Quráni tukufu, pamoja na mradi wa semina endelevu za Quráni hapa mkoani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: