Kuanza kwa shindano la (Pambo la Dini) la kielimu

Maoni katika picha
Kitengo cha masomo ya Quráni katika chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza kwa shindano la kielimu lililo pewa jina la (Pambo la Dini) kwa wanawake awamu ya kwanza, na kutoa wito kwa watafiti wa kike katika sekta ya Quráni wajitokeze kushiriki kama ilivyo bainishwa na rais wa chuo kikuu Shekh Hussein Turabi, miongoni mwa mada za shindano hili ni:

  • - Njia za kufuata maelekezo ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani kwa vijana wa kiislamu.
  • - Athari nzuri ya kujifunza Quráni tukufu na kuihifadhi kwa wanajamii.

Masharti ya kushiriki ni:

  • - Utafiti usiwe umeshawahi kusambazwa.
  • - Usiwe chini ya kurasa (15) na zisizidi (20).
  • - Uandikwe kwa program ya (word) hati ya (Arial) ukubwa wa maandisi saizi 14.
  • - Usiwe na makosa ya kinahau, kiuandisi na kilugha kwa ujumla.
  • - Uambatanishwe na wasifu (cv) ya muandishi na namba ya simu yake.

Tafiti zote zitakabidhiwa kwa kamati ya majaji itakayo husika na kuzichuja na kuzifanyia marekebisho.

Akaendelea kusema: “Washiriki watapewa vyeti vya ushiriki na washindi watatu wa mwanzo watapewa zawadi, mwisho wa kupokea tafiti hizo ni (1 Dhulqaadah 1442h), kushiriki kwenye shindano au maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe ifuatayo (Quraani_Studies@)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: