Kumbukumbu ya uvunjwaji wa makaburi ya Baqii

Maoni katika picha
Mwezi nane Shawwal ni siku ya kukumbuka jinai mbaya iliyofanywa na mikono ya maadui wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ya kuvunja makaburi ya Maimamu waongofu (a.s) na kutweza heshima yao na utukufu wao.

Makaburi ya Baqii Gharqad yanaidadi kubwa ya maswahaba na watu wa familia ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na waislamu wa kawaida, wakiwemo Maimamu wane ambao ni: (Imamu Hassan bun Ali Azzakii, Imamu Ali bun Hussein Asajjaad, Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir, Imamu Jafari bun Muhammad Aswaadiq –a.s-).

Kuna mashambulizi mawili yaliyofanywa kufuta athari za makaburi hayo matakatifu:

Kwanza: mwaka (1220h / 1805m) kisha waislamu wakayajenga upya katika muonekano mzuri baada ya kushika uongozi utawala wa Othumaniyya, wakajenga kubba na misikiti kwa umaridadi mkubwa, waislamu wakawa wanaenda kufanya zaira kwenye makaburi hayo.

Muengereza mmoja aliusifu mji wa Madina baada ya kujengwa upya kuwa unafanana na Stambul au ukosawa na miji mingine mizuri duniani, huo ulikua mwaka (1877 – 1878m).

Pili: mwaka (1344h / 1925m) kwa mara nyingine maadui walivamia Baqii na kuvunja majengo matakatifu ya Maimamu watukufu (a.s) na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), Baqii ikawa jangwa, kiasi huwezi kujua mahala penye kaburi au kujua muhusika wa kaburi.

Msafiri wa Moroko (Eldowan Ritar) anauzungumzia mji wa Madina baada ya jinai ya pili iliyofanywa na Mawahadi wakati walipo uteka mji wa Madina na kuuwa maelfu ya waumini: “Mji ulivunjwa na kuporomoshwa kubba nyeupe zilizo kuwa zinaashiria makaburi ya watu wa nyumba ya Mtume.. na makaburi mengine yote yalivunjwa na kusawazishwa na udongo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: