Kila mwaka katika siku ya mwezi nane Shawwal hufufuka huzuni za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), kwa kukumbuka jinai mbaya zilizo fanywa na mikono ya madhalimu na maadui zao, ya kuvunja makaburi ya Maimamu waongofu (a.s) na kuondoa heshima na utukufu wao.
Katika kuomboleza na kukumbuka jinai hizo, huzuni imetanda ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kuta za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimewekwa mapambo meusi, kazi hiyo imefanywa na watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram kwa kushirikiana na kitengo cha zawadi na nadhiri kupitia idara ya ushonaji iliyo chini yake. Zimewashwa taa nyekundu zinazo ashiria huzuni, na mabango yenye jumbe zinazo ashiria huzuni na kukumbusha tukio hilo yamewekwa juu ya kuta, kama sehemu ya kukumbuka tukio hili chungu na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Kumbuka kuwa siku ya mwezi nane Shawwal ni suku ya kukumbuka kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu (a.s) waliozikwa Baqii: Imamu Hassan Almujtaba mtoto wa kiongozi wa waumini, Imamu Ali bun Hussein Zainul-Aabidina, Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir na Imamu Jafari Swadiq mtoto wa Imamu Baaqir (a.s), nayo ni kumbukumbu ya mwaka wa tisini na nane tangu maadui wa Ahlulbait (a.s) walipovunja makaburi hayo matakatifu.