Mashamba ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanamchango mkubwa wa kujitosheleza katika sekta ya kilimo

Maoni katika picha
Kitengo cha kilimo na bidhaa za wanyama chini ya shirika la kiuchumi Alkafeel, ambalo ni miongoni mwa mashirika ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesema kuwa mashamba yake yamechangia kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa mazao ya kijani yanayo hitajika kwa kiwango kikubwa na wananchi, sambamba na kubadilisha eneo kubwa la jangwa kuwa kijani kibichi na sehemu bora ya kilimo.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Ali Muzáli Laaidh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kilimo ni sekta inayopewa kipaombele na Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kuiwekea miundombinu wezeshi ikiwa ni pamoja na rasilimali watu na rasilimali vitu, kwa ajili ya kuzalisha mazao yanayo hitajika zaidi hapa nchini na kutengeneza ajira kwa watu wengi zaidi wasiokuwa na kazi”.

Akaongeza kuwa: “Mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi na mashamba ya Haamilu Liwaa (a.s), ni moja ya miradi inayojenga uwezo wa kujitegemea na mfano hai wa kubadilisha jangwa kuwa ardhi ya kijani inayofaa kwa kilimo, nayo ni mashamba ya kisasa zaidi, yamelimwa kwa kutumia teknolojia inayotumiwa na nchi zilizo endelea, kuanzia uandaaji wa mbegu, vitalu, upandaji hadi umwagiliaji na njia zinazo tumika kupambana na maradhi ya mimea, dawa zoto zinazotumika ni rafiki kwa mazingira, aidha kilimo kinazingatia mahitaji ya soko katika kila msimu”.

Akasema: “Mashamba yana aina tofauti za mazao yanayo hitajika zaidi na wananchi, kwa mfano: Tomate, Bilinganya, Viazi mbatata, Tango, Pilipili baridi na pilipili kali, Nyanya chungu, Tikiti maji, Bamia pamoja na aima mbalimbali za mboga za majani na vitunguu vyekungu na vyeupe, mazao yote yanapamba vizuri tena ndani ya muda mfupi na yanaubora wa kimataifa, yanazidi mazao ambayo hutoka nje ya nchi kwa ubora na utamu, pamoja na uimara wake wa kujikinga na bakteria na uhimili wa hali ya hewa ya Iraq”.

Kumbuka kuwa mashamba yapo katika barabara ya (Karbala – Najafu) karibu na nguzo namba (1145), mazao yote yanapatikana kwenye maduka ya shirika la Nurul-Kafeel ndani na nje ya Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: