Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati kinaangazia mitazamo ya Abdulkarim Sarush

Maoni katika picha
Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeangazia mradi wa kielimu wa Abdulkarim Sarush, kutokana na misingi yake na mitazamo yake, kwa kuchapisha toleo la tano katika mfululizo wa vitabu vya (mtazamo wa kisasa).

Mkuu wa kituo hicho Sayyid Hashim Milani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitabu cha (Abdulkarim Sarush ni tafiti za kinadhariyya na uhalisi) ni muhimu katika kituo, kazi hiyo imefanywa na jopo la watafiti katika kuangalia mitazamo ya wanachuoni katika ulimwengu wa kiislamu”.

Akaongeza kuwa: “Katika swala hili mara nyingi huangaliwa mwenendo wa upatikanaji wa fikra chini ya anuani isemayo (mfumo anzilishi) kwa kutafiti na kuchambua mafanikio ya fikra za sasa na kuangalia mambo yanayofaa”.

Akafafanua kuwa: “Sehemu hii huhusisha tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuangazia fikra za Abdulkarim Sarush, tambua kuwa huyo ni katika waandishi wakubwa, ameandika vitabu vingi vinavyo husu swala hilo, tutaanza na hatua ya kwanza katika kuangazia fikra ya Abdulkarim Sarush, kwa kuangalia historia yake na misingi yake pamoja na mitazamo yake”.

Akamaliza kwa kusema: “Katika hatua ya pili tutabainisha utowaji wa maoni na mitazamo yake, tutafanya tafiti zitakazo saidia kuonyesha uhalisia zitakazo saidia kubaini mafanikio au kufeli katika uwanja wa msingi wa utamaduni wa kiislamu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: