Semina ya kujenga uwezo wa namna ya kuripoti habari za kimalezi

Maoni katika picha
Idara ya habari za malezi katika kitengo cha malezi na elimu ya juu, inaendesha mafunzo maalum ya njia za kuripoti habari zinazo husu malezi, kwa watumishi wa habari waliopo kwenye shule za Al-Ameed.

Mkufunzi wa semina hiyo mwanahabari Salaam Banai amesema kuwa: “Mafunzo yamejikita katika misingi ya uandishi wa habari za malezi na malengo yake”.

Akaongeza kuwa: “Tumeangalia kwa urefu namna ya kuhariri habari zenye umuhimu mkubwa katika uandishi, kuanzia uandishi, uhariri na utangazaji”.

Akabainisha kuwa: “Mihadhara ya semina imepambwa na vipengele vya mazowezi ya vitendo yaliyo onyesha uwelewa wa washiriki, na mwisho wa semina kutakuwa na mtihani kwa washiriki wote, ili kupima uwelewa wao”. Akasema: “Lengo la semina hii ni kujenga uwezo wa kuandika habari na kufanya uhariri kwa watumishi, hasa habari zinazo husu malezi na majarida ya shule”.

Naye Ustadh Yusufu Twaaiy kiongozi wa idara ya habari za malezi katika kitengo hicho amesema: “Kutokana na umuhimu walionao watumishi wa idara ya habari kwenye taasisi yetu ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, daima tunazingatia kuongeza vipaji na uwezo wao ili kuboresha sekta ya habari”.

Akaongeza kuwa: “Hii sio semina ya kwanza, tumesha fanya semina nyingi za waandishi wa habari kama zinavyo fanya taasisi kubwa za habari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: