Kumbukumbu ya kuuwawa kishahidi kwa Hamza bun Abdulmutwalib simba wa Mwenyezi Mungu na Ammi wa Mtume wake

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi kumi na tano Shawwal, mwaka wa tatu hijiriyya Mtume (s.a.w.w) alihuzunika sana, kwa kifo cha Ammi yake Hamza bun Abdulmutwalib (r.a), katika vita ya Uhudi kati ya waislamu na washirikina.

Imepokewa kutoka kwa Imamu Ridhwa kutoka kwa baba zake (a.s), kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) anasema: (Ndugu yangu bora ni Ali na Ammi yangu bora ni Hamza na Abbasi).

Hamza alishiriki vita ya Uhudi akiwa na umuhimu maalum, kwa sababu aliuwa viongozi wa waarabu katika vita ya Badri, aliwapa majonzi na huzuni kubwa washirikina wa Maka, wakamuandalia njama ya kulipiza kisasi, Hindu bint Utba alikuwa amemuandaa Wahshi bun Harbu mlenga shabaha bingwa kwa ajili ya vita hiyo, alikuwa ni mtumwa kutoka Habeshi (Ithiopia), akamuahidi mali nyingi kama akifanikiwa kumuua Hamza, kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kuuwawa kwa baba yake na kaka yake katika vita ya Badri.

Wahshi alipokua katika ardhi ya Uhudi alisema: Hakika mimi namuona Hamza anapiga watu kwa upanga wake, kila mtu anayesogea mbele yake anamuuwa kwa upanga, nikashika vizuri mkuki wangu na kumtupia, ukamchoma kiunoni kwake akaanguka kisha askari wakammalizia, Hindi alipopewa taarifa ya kifo cha Hamza (a.s), alikuja akakata ini lake na kuliweka mdomoni mwake, lakini hakuweza kutafuna akatema.

Baada ya kuisha vita muili wa Hamza (a.s) ulikutwa juu ya udongo ukiwa umekatwa katwa, Mtume (s.a.w.w) alipouona alilia kisha akasema: (Sitopata msiba mkubwa kama msiba wako, sijawahi kusimama mahala pazito kwangu kama mahala hapa), Mtume (s.a.w.w) akaamuru azikwe.

Mtume (s.a.w.w) alisema maneno ya kuhuzunisha, tunataja baadhi ya maneno hayo: “(Ewe Ammi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, simba wa Mwenyezi Mungu na simba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.. Ewe Hamza ewe mfanya wema, ewe Hamza ewe msaidiaji wenye matatizo, ewe Hamza ewe ngao ya Mtume (s.a.w.w): Amani iwe juu yako ewe Ammi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na mbora wa mashahidi, amani iwe juu yako ewe simba wa Mwenyezi Mungu na simba wa Mtume wake, nashuhudia kuwa umepigana jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ulikuwa na roho nzuri, umetafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na umependa neema zilizopo kwa Mwenyezi Mungu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: