Unatambua nini kuhusu marashi ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na nini tofauti yake?

Maoni katika picha
Zaairu anapoingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hupokelea na marashi ya Imani, moyo hulainika kwa aya za Quráni na dua, huwa yupo miongoni mwa nyumba alizo ruhusu Mwenyezi Mungu litajwe jina lake, humfanya kufungamana na rehema za Mwenyezi Mungu anapokuwa katika mazingira hayo, mara harufu nzuri ya marashi hunukia katika roho yake.

Watumishi wa idara ya usimamizi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa kazi wanazo fanya ni kufukiza na kuweka marashi ndani ya haram na kwenye korido zake, kupitia idara ya ufukizaji na marashi iliyo chini yake.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Nizaar Khaliil Ghina ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Idara yetu hufukiza na kuweka marashi ndani ya haram takatifu, kwa kufuata ratiba maalum, tunatumia marashi bora ya kienyeji, rafiki kwa mazingira na hukaa muda mrefu, harufu yake inaendana na mazingira ya kiroho yaliyopo ndani ya haram tukufu, yapo ya aina mbili ya maji na magumu, pamoja na harufu nzuri lakini pia ni sumu ya bakteria wala haukeri kwa yeyote na inaendana na utukufu wa sehemu hii”.

Akaongeza kuwa: “Marashi ya maji hutengenezwa kwa malighafi za kienyeji, asilimia kubwa ni mauwa ya kawaida, na bukhuri (ubani) ni mzuri sana unatoka Asia mashariki, huchanganywa kati ya bukhuri (ubani) wa asili na vijiti vyenye harufu nzuri”.

Akafafanua kuwa: “Ufukizaji huhusisha kuta, ardhi na miswala pamoja na dirisha la malalo takatifu, kazi zote hufanywa kwa kutumia vifaa maalum au kwa mkono”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: