Arshu-Tilaawah imeanza utaratibu wake wa usomaji wa Quráni

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni katika Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimeanza kufanya zikao vya usomaji wa Quráni ndani ya haram tukufu, baada ya kusimama katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mahafali imeshuhudia usomaji wa Quráni na mihadhara ya kidini, Quráni imesomwa na msomaji wa Ataba Faisal Matwar Sharifi, Faaris Hamdani kutoka Mosul, Dokta Munjidi Kaabi ameeleza fani tofauti za Quráni kupitia mada isemayo (kutakasa nafsi).

Tambua kuwa hafla imerushwa mubashara na chanel ya Quráni chini ya kituo cha luninga cha Karbala, na kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tambua kuwa Maahadi ya Quráni tukufu na matawi yake yote, ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kusambaza elimu ya Quráni na kuandaa jamii inayofuata mafundisho ya Quráni na yenye uwezo wa kufanya tafiti katika sekta tofauti kwa kutumia Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: