Watumishi Masayyid ni pambo la kihistoria na muendelezo wa babu zao katika utumishi

Maoni katika picha
Idara ya watumishi Masayyid chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa idara zenye umaalum wake na umuhimu mkubwa pamoja na utukufu wao wa kufungamana na nasaba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Ili kutambua vyema kuhusu idara hiyo na jukumu lake katika kuwatumikia mazuwaru watukufu, Sayyid Hashim Shami ameongea na mtandao wa Alkafeel akasema kuwa: “Watumishi wa idara hii wanazaidi ya jukumu moja, ukizingatia kuwa wengi wao wanaendeleza huduma zilizokuwa zikitolewa na babu zao katika eneo hili takatifu, aidha mazuwaru wamezowea kumuona mtoa huduma wa Ataba akiwa katika muonekano maalum, vazi la Masayyid ni miongoni mwa mambo yanayo onyesha uwepo wao katika Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa kazi zinazo fanywa na watumishi wa idara hiyo ni:

  • - Kuandaa sehemu za kupumzika mazuwaru na kusimamia usafi na twahara ya sehemu hizo, pamoja na kutandika miswala ndani ya Atabatu Abbasiyya na maeneo yote ya haram takatifu, jukumu hilo huongezeka katika siku za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu na katika siku za matukio maalum ya kidini, kama vile sikukuu za Iddi, siku za Lailatul-Qadr na siku za Alkhamisi na Ijumaa na zinginezo
  • - Kusoma ziara tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku kwa niyaba ya kila anayeomba huduma hiyo kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel, pamoja na kuwasomea watu wenye mahitaji maalum na kila mtu anayeomba kusomewa katika mazuwaru, sambamba na kusomea jeneza na kuongoza swala ya maiti kama wakiombwa na wafiwa, na kusoma ziara hiyo wakati wa kufungua dirisha la kaburi na kwenye matukio mengine.
  • - Kudumisha usafi kwenye kabati za vitabu na kupanga vizuri vitabu kila aina na sehemu yake, na kuondoa vitabu vilivyo chanika na kuchakaa pamoja na kurekebisha kabati inapoharibika.
  • - Kufukiza na kupuliza marashi hususan karibu na wakati wa swala na siku za matukio ya kiduni.
  • - Kusimamia matembezi ya mazuwaru watukufu na mawakibu za waombolezaji.
  • - Kuhuisha matukio ya kidini ya furaha na huzuni kwa Ahlulbait (a.s) pamoja na kusaidia upambaji wa dirisha la kaburi tukufu kwa kuweka mauwa wakati wa furaha na kuweka mapambo meusi wakati wa msiba”.

Akaongeza kuwa: “Kunaushirikiano mkubwa kati ya idara ya Masayyid, kitengo cha mahusiano na kitengo cha Dini, katika kupokea wageni na kuitikia mialiko inayoletwa Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kushiriki kwenye makongamano na nadwa zinazo fanywa ndani na nje ya Ataba, pamoja na kufungua na kufunga milango ya haram tukufu inapo hitajika, hasa wakati wa kudeki haram takatifu”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi zetu hazina mpaka, tunashirikiana na vitengo vyote vinavyo toa huduma katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani lengo letu ni kufanikisha utoaji bora wa huduma kwa mazuwaru watukufu, heshima na utukufu wa watumishi wa idara hii ni kutoa huduma sawa na watumishi wengine wa haram takatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: