Kamati ya wakuu wa vyuo vya meno nchini Iraq imesema kuwa chuo kikuu cha Alkafeel ni mfano mwema wa kielimu hapa Iraq, tunafaa kujivunia na kupongeza kazi nzuri wanazofanya, hayo yamesemwa baada ya kamati hiyo kutembelea chuo hicho.
Rais wa chuo Dokta Duniya Wadii Sabú amesema: “Chuo kikuu cha Alkafeel ni kitovu cha elimu, na kinasifa zote za kielimu, jambo hili sio geni kwa mradi wowote unao simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akasisitiza kuwa: “Kamati imeangalia vitengo vya chuo kikuu Alkafeel hususan kitengo cha famasia, kumbi za madarasa, maabara pamoja na mfumo wa elimu unaotumiwa na chuo hicho na majengo yake”.
Kumbuka kuwa: “Chuo kikuu cha Alkafeel katika mkoa wa Najafu kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimekuwa kikiboresha mfumo wa elimu wakati wote na kufanya harakati za kielimu, kitamaduni na kimalezi pamoja na tafiti za kielimu hapa Iraq”.