Kituo cha turathi za Hilla kimechapisha toleo la pili la hakiki za Hilla

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha toleo la pili katika hakiki za Hilla.

Toleo hili limehusisha (kufanyia uhakiki kitabu cha Aarifu wa Nahalul-Ghaarifu- cha Shekh Muhammad Salmaan Nuhu Kaabi na Hamadi Nuhu), kazi hiyo imefanywa na mhakiki Dokta Mudhwaru Selemani Alhilliy, pamoja na kuhakikiwa na kituo cha turathi za Hilla.

Tumeongea na mkuu wa kituo Shekh Swadiq Khuwailidi kuhusu toleo hili, amesema: “Mradi wa (kuandika hakiki za mji wa Hilla) ni miongoni mwa miradi mikubwa inayo fanywa na kituo hiki, kiliandika toleo la kwanza, lililokuwa na mafanikio makubwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na hili ni toleo la pili katika mfululizo huo, limetokana na kitabu cha mshairi wa Hilla (Hamadi Nuhu Kaabi), ambaye mashairi yake yanafanana na mashairi ya waarabu wa zamani, kama mashairi ya Radhiyya na Murtadha”.

Akaongeza kuwa: “Turathi za Hilla ni miongoni mwa vituo muhimu kielimu, kinacho shajihisha ubunifu, uandishi, uhakiki na usambazaji hapa Iraq, kitaendelea kufanya kila kiwezalo kwa ajili ya kuonyesha turathi za taifa hili tukufu”.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Hilla kinamachapisho mengine pia, kimejikita katika kuchapisha vitabu vinavyo eleza turathi za Dini, elimu, maarifa ya kijamii hususan yanayo husiana na mji wa Hilla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: