Kuratibu na kuendesha semina za Quráni kwa wanafunzi wa chuo

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa semina iitwayo (Albayyinaat) kwa wanafunzi thelathini wa vyuo, inayo husu kuwafundisha usomaji na hukumu za tajwidi kwa ajili ya kuwaandaa waweze kushiriki kwenye semina zingine za Quráni zijazo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi kwa mtandao wa Alkafeel, amesema kwa: “Hii ni moja ya semina nyingi zinazo tolewa na Maahadi kwa kuhudhuria wanasemina au kwa njia ya mtandao, semina hizi zinalenga kufundisha usomaji sahihi wa Quráni tukufu, na kuangalia misingi ya tajwidi, pamoja na kutamka kwa ufasaha herufi za Quráni na baadhi ya hukumu za lazima katika usomaji wa Quráni tukufu, inasimamiwa na wasomi walio bobea kwa kufuata ratiba maalum”.

Akaendelea kusema: “Tunatarajia washiriki watanufaika na semina hii kwa kukijua vilivyo kitabu kitakatifu na kujiandaa na hatua ifuatayo ya kuhifadhi Quráni tukufu, ndio maana Maahadi inalipa umuhimu wa pekee swala hili”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inalenga kutoa elimu ya Dini kwa wanawake, ikiwemo elimu hii ya “Maarifa ya Quráni”, na kutengeneza kizazi cha wanawake wanaofanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu na wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta tofauti za masomo ya Quráni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: