Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda katika korido za Atabatu Abbasiyya tukufu na kuta zake, kwa ajili ya kuonyesha huzuni ya kifo cha Imamu Abu Abdillahi Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) kinacho sadifu siku ya Jumatatu (25 Shawwal 1442h) sawa na tarehe (7 Juni 2021m).

Vitambaa vilivyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni vimewekwa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni sehemu ya kuonyesha huzuni kwa watumishi wa Ataba na kumpa pole Mtume mtukufu na watu wa nyumbani kwake (a.s) kutokana na msiba huu, unao umiza roho za wapenzi na wafuasi wao, kwa nini isiwe hivyo wakati ni mhimili madhubuti na mkweli wa familia, Imamu mtakasifu wa sita katika Maimamu watakatifu waliotajwa na Mtume (s.a.w.w) kuwa viongozi baada yake.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba ya maombolezo inayo endana na mazingira ya sasa, kutakuwa na majlisi ya kuomboleza asubuhi na jioni pamoja na shughuli zingine za uombolezaji.

Kumbuka kuwa mwezi ishirini na tano Shawwal mwaka (148) hijiriyya, watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao, walipata msiba kwa kufiwa na Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) Imamu wa sita, katika Maimamu watakatifu waliotajwa na Mtume (s.a.w.w), Muda wa Uimamu wake ulikua miaka (34), alizaliwa katika mji wa Madina na akafa katika mji huo akiwa na miaka (65 au 68), akazikwa katika makaburi ya Baqii pembeni ya kaburi la baba yake Imamu Baaqir na babu yake Imamu Sajjaad na Imamu Hassan (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: