Wito wa kushiriki kwenye nadwa ya kielimu kuhusu idara za malezi kwa Imamu Swadiq (a.s)

Maoni katika picha
Shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu zinatoa wito wa kushiriki kwenye nadwa ya kielimu iliyopewa jina la (Idara za malezi kwa Imamu Jafari Swadiq (a.s) katika kivuli cha changamoto) chini ya uhadhiri wa Sayyid Muhammad Abdullahi Mussawi na usimamizi wa rais wa kitengo Dokta Ahmadi Swabihi Kaabi, kuanzia saa mbili jioni siku ya Jumatatu (25 Shawwal 1442h) sawa na tarehe (7 Juni 2021m) kupitia mtandao wa (ZOOM) kwa link ifuatayo: https://us02web.zoom.us/j/3740873005

Tambua kuwa nadwa hii ni sehemu ya mfululizo wa masomo ya kimalezi na kielimu hapa nchini, itahusu mambo tofauti katika idara ya malezi kwa Imamu Swadiq (a.s) zinapotokea changamoto katika jamii, tutajadili baadhi ya kauli zake na hadithi zinazo husu mada hiyo pamoja na kanuni za malezi na maadili za kimataifa, zinazo endana na falsafa ya maudhui ya malezi, pamoja na mambo mengine yanayo endana na anuani ya mhadhara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: