Balaza la mji wa Karbala limeuzawadia uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Baraza la mji wa Karbala limeupa zawadi uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar, kutokana na kazi kubwa wanayo fanya ya kuhudumia mazuwaru na wakazi wa mji huu.

Tumeongea na rais wa balaza la mji wa Karbala Sayyid Yusufu Aali-Maajid kuhusu zawadi hiyo, amesema kuwa: “Kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na utekelezaji wa katibu mkuu na watumishi wake, tumeona maendeleo makubwa katika miradi mbalimbali wanayo fanya kwa ajili ya kuwatumikia wakazi wa Karbala na wairaq kwa ujumla”.

Akaendelea kusema: “Sisi katika balaza la mji wa Karbala tunaona vyema maendeleo mazuri katika miradi inayofanywa na Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Tunapongeza kazi nzuri inayofanywa na Atabatu Abbasiyya na tunawaombea mafanikio mema watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru watukufu pamoja na wakazi wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: