Kituo cha miradi ya Quráni kinafanya semina ya sauti na naghama

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinafanya semina ya sauti, naghama na hukumu za usomaji wa Quráni, pamoja na masomo ya maarifa ya Quráni na Akhlaqi.

Washiriki wa semina hiyo ni zaidi ya wanafunzi (30) wasomaji wa Quráni na waimbaji kutoka idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari za Ataba takatifu.

Wakufunzi wa semina hiyo ni walimu wa kituo waliobobea katika usomaji wa Quráni na hukumu zake, wamefafanua masomo tofauti yanayo husu sauti na naghama za Quráni pamoja na masomo ya Akhlaq ambayo ndiyo msingi wa mwenendo wa vizito viwili.

Tunatarajia kuwa semina itaendelea kwa kufundisha siku tatu katika kila wiki ndani ya jengo la Shekh Kuleini.

Tambua kuwa Maahadi ya Quráni tukufu ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha masomo ya Quráni, na kutengeneza jamii inayofanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu, inayo weza kufanya tafiti za kielimu katika fani tofauti za Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: