Kifo cha mkweli wa Aalu-Bait (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) na wapenzi wao pamoja na wafuasi wao katika siku kama ya leo, mwezi ishirini na tano Shawwal mwaka (148) walipata msiba wa kufiwa na Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s), Imamu wa sita katika Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), babu yake Mtume mtukufu (s.a.w.w) ndiye aliye mpa jina la Swadiq.

Jina lake kamili ni Jafari bun Muhammad Albaaqir (a.s), na mama yake ni Farwah binti Qassim bun Muhammad bun Abubakari ajulikanae kwa jina la Mukarramah, aliishi (a.s) katika zama za utawala wa bani Umayya, alishuhudia kuanguka kwa utawala huo, alipata maudhi na vitimbi kutoka kwa Saffaah Jafari Mansuur, ambaye alimuandama Imamu (a.s) hadi akamuuwa kwa sumu mwezi ishirini na tano Shawwal mwaka wa (148) hijiriyya.

Historia inaonyesha kuwa Imamu Swadiq (a.s) alifanyiwa maudhi mengi na khalifa wa bani Abbasi Mansuur, alimtaka mara nyingi atoke Madina na kwenda Iraq kwa lengo la kumuuwa, lakini alikuwa anashindwa kumuuwa kutokana na karama alizokuwa anaziona kwa Imamu (a.s), jambo ambalo liliendelea kumpa hofu ya utawala wake, akaanza kupanga mbinu za kummaliza, ndio akaamua kumuwekea sumu kali kwenye zabibu, baada ya Imamu (a.s) kula zabibu hizo sumu ikakata kata maini yake na ikawa sababu ya kifo chake (a.s), baada ya kufa akasimama mtoto wake Imamu Mussa bun Jafari (a.s) kuandaa muili wa baba yake kama alivyo husiwa, kisha wakabeba jeneza lake kwenda kumzika, akatangulia Abuhuraira Ajaliy akasema:

Nasema hakika wameondoka wakiwa wamembeba * juu ya mabega na mashingo yao.

Mnajua mmebeba nani kwenda kuzika * mja mwema mbora kushinda wote.

Wakaenda kumuweka ndani ya kaburi lake * na wakamfunika kwa udongo na kumuacha.

Alizikwa (a.s) katika makaburi ya Baqii pamoja na babu yake upande wa mama yake Imamu Hassan na babu upande wa baba Imamu Zainul-Aabidina, na baba yake Baaqir (a.s), naye ni Imamu wa mwisho kuzikwa katika makaburi hayo, watoto wake walizikwa Iraq, ispokua Imamu Ridhwa (a.s) alizikwa Khurasani.

Baada ya kumaliza umri wake kwa kufundisha na kufanya ibada mjukuu huyu wa Mtume (s.a.w.w) Jafari Swadiq (a.s) aliaga dunia, hakika alikuwa Aalimu mkubwa mwenye zuhudi, mtetezi wa haki na uadilifu, mlinganiaji katika njia ya Mwenyezi Mungu mtukufu, mtenda wema pia aliamrisha wema na kukataza mabaya, aliuonyesha umma njia sahihi.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayo fufuliwa kuwa hai, wamefaulu watakao fuata uongofu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: