Kuomboleza kifo cha kiongozi wa wakweli (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s), kwa kufanya majlisi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa muda wa siku mbili, kila siku kulikuwa na muhadhara mmoja ulio hudhuriwa na mazuwaru pamoja na watumishi wa malalo takatifu.

Mzungumzaji alikuwa ni Shekh Majidi Sultani, ameongea vitu vingi kuhusu uhai wa Imamu Swadiq (a.s) pamoja na elimu yake na mazingira aliyo ishi, yaliyo msaidia kufikisha mafundisho ya Dini na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), na namna alivyo weza kuendeleza mafundisho ya Dini baada ya kifo cha baba yake Imamu Baaqir (a.s) katika kipindi cha uongozi wake uliodumu kwa muda wa miaka thelathini na nne, alilea wanachuoni wengi na mafaqihi wema wanaofuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s), akafanikiwa kulinda misingi ya madhehebu ya Ahlulbait (a.s).

Majlisi ikafungwa kwa kusoma tenzi za maombolezo zilizo amsha hisia ya huzuni ya msiba huu, ambao ni miongoni mwa matukio makubwa katika ulimwengu wa kiislamu, vilio vilisikika kila sehemu, watu wakamiminika katika nyumba ya Imamu wakiwa wanabubujikwa machozi, kwani alikuwa tegemeo na kimbilio la kila muislamu.

Kumbuka kuwa mwezi ishirini na tano Shawwal mwaka wa (148) hijiriyya, watu wa nyumba ya Mtume na wafuasi wao walipata msiba kwa kufiwa na Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s), Imamu wa sita katika Maimamu watakatifu wa nyumba ya Mtume (a.s) waliobashiriwa na Mtume (s.a.w.w), kipindi cha Uimamu wake kilikuwa miaka (34), alizaliwa katika mji wa Madina na alikufa katika mji huo akiwa na miaka (65 au 68) kutokana na ikhtilafu ya riwaya, akazikwa katika makabuli ya Baqii pembeni ya baba yake Imamu Baaqir, na babu yake Imamu Sajjaad, na Imamu Hassan (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: