Maahadi ya Quráni tukufu katika mji wa Najafu imezindua semina ya hukumu za tajwidi

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imezindua semina ya hukumu za tajwidi na usomaji sahihi wa Quráni, ikiwa na washiriki zaidi ya (50) kutoka Najafu, itafanywa kwa wanafunzi kuhudhuria darasani siku mbili kwa wiki.

Sayyid Muhandi Majidi Almayali kiongozi wa Maahadi hiyo amesema kuwa: “Tawi letu limezowea kufanya semina mbalimbali kuhusu Quráni katika kipindi chote cha mwaka”.

Akaongeza kuwa: “Semina hii inafanywa baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, baada ya watu kutambua umuhimu wa kusoma Quráni kwa usahihi”.

Akaendelea kusema: “Mkufunzi wa semina hii ni Ustadh Ahmadi Zamili, ni moja ya semina nyingi zinazo endeshwa na Maahadi, kwa lengo la kufundisha usomaji sahihi wa Quráni tukufu na kusahihisha makosa katika usomaji pamoja na kusoma kwa kufuata hukumu za tajwidi”.

Kumbuka kuwa semina zinazo fanywa na Maahadi ya Quráni tukufu ni moja ya harakati muhimu za Maahadi, zinapewa kipaombele zaidi na zinamuitikio mkubwa, tayali watu wengi wamehitimu katika semina hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: