Wanawake waomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameandaa majlisi ya wanawake ya kuomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s), maombolezo hayo hufanywa kila mwaka ndani ya Sardabu ya Imamu Kaadhim (a.s) katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na mazuwaru pamoja na wakinadada wa Zainabiyaat miongoni mwa watumishi wa malalo hiyo takatifu.

Makamo kiongozi wa idara ya wanawake bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maombolezo haya hufanywa kila mwaka chini ya harakati za idara, huwa mstari wa mbele katika kuomboleza vifo vya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), kutokana na kuwepo kwa janga la Korona, mwaka huu tumehusisha idadi chache ya mazuwaru pamoja na wahudumu wachache wa malalo takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Majlisi ilikuwa na muhadhara kuhusu nafasi ya pekee aliyokuwa nayo Imamu Swadiq (a.s), na kubainisha hukumu za Dini na kueleza namna alivyo fanikiwa (a.s) kufundisha Dini, mafundisho yake yameendelea kuwa nuru inayo angaza hadi leo, hali kadhalika zikazungumzwa dhulma alizo fanyiwa na viongozi wauvu wa zama zake, alinyanyaswa na kuwekewa vizuwizi mbalimbali pamoja na kueleza namna alivyo pambana na vizuwizi hivyo kwa kufanya subira na kutumia hekima, kisha zikasomwa tenzi zilizo amsha hisia za huzuni ya msiba”.

Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri wa kike hufanya majlisi za maomboleza katika kukumbuka vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: