Watumishi wa Maahadi ya Alkafeel ya watoto wafanya warsha

Maoni katika picha
Kitengo ya malezi na elimu kimeandaa warsha kwa watumishi wa Maahadi ya Alkafeel ya watoto, wanafundishwa misingi ya fikra za kielimu katika mfumo wa Quráni.

Kiongozi wa idara ya maelekezo Ustadh Falahu Hassan Juma amesema: “Tumeandaa warsha hii kwa ajili ya kuongeza elimu kwa watumishi wa Maahadi, na uwezo wa nadhariya za malezi na elimu za kisasa”.

Akaongeza kuwa: “Warsha hii ni sehemu ya utaratibu wa kitengo cha malezi na elimu ya juu wa kuongeza uwezo wa watumishi wa Maahadi, inafanywa chini ya anuani isemayo: (Mkakati wa kubadili tabia kwa mujibu wa Quráni tukufu), nayo ni msingi wa warsha zitakazo endelea kufanywa”.

Akasema kuwa: “Sehemu ya kwanza ya warsha tumeangalia upande wa nadhariyya”.

Akafafanua kuwa: “Katika warsha zijazo tutaangalia upande wa vitendo na namna ya kubadilisha mwenendo kwa dalili za ara za Quráni tukufu, ili iwe rahisi kufanyiwa kazi na watoto katika Maahadi, na kuhakikisha wanakuwa na tabia njema na kuacha tabia mbaya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: